Afisa Mtendaji Mkuu wa TAFICO, Dkt. Suleiman Kiula, ndc (T), akisaini makubaliano ya ujenzi wa meli mbili za uvuvi wa Bahari Kuu, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Agosti 24, 2026 jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TAFICO, Dkt. Suleiman Kiula, ndc (T), akipokea Nishani ya Kumbukumbu kutoka kwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji, Rear Admiral Ameir Ramadhani Hassan, alipofanya ziara ya kikazi katika Makao Makuu ya Kamandi ya Jeshi la Wanamaji, Kigamboni, Dar es Salaam, Septemba 23, 2026.
TAFICO FV. 01, Meli ya kwanza ya uvuvi wa Bahari Kuu ya TAFICO ikiwa imeegeshwa katika gati la TAFICO lililopo Ras Mkwavi, Kigamboni, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (kulia kwake), Naibu Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Mhe. Mboja Ramadhan Mshenga (kushoto kwake), na mabaharia wakati wa hafla ya uzinduzi wa meli ya kwanza ya uvuvi wa Bahari Kuu ya TAFICO.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua meli ya kwanza ya Uvuvi wa bahari kuu ambayo itaiwezesha nchi kuvua samaki waliopo kwenye ukanda wa maalum wa uchumi wa bahari (EEZ) ambao awali haukuweza kufikiwa kutokana na kukosekana kwa meli ya aina hiyo.

Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo katika Makao Makuu ya TAFICO Ras Mkwavi, Kigamboni Dar es Salaam iliyofanyika 13 Machi 2026
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (katikati) kwenye picha ya pamoja na viongozi na watendaji wa wizara, menejimenti na watumishi wa TAFICO, alipotembelea Makao Makuu ya TAFICO Disemba 05, 2025

Jodari (Yellowfin tuna): moja ya aina ya samaki ambazo TAFICO inalenga kuvua kutoka maji marefu ya bahari, kuchakata, kuuza na kuongeza mnyororo wa thamani