Huduma ya Maghala ya Ubaridi
Ghala la Ubaridi
Ghala la Ubaridi la kuhifadhia samaki ni miongoni mwa vifaa maalum katika Sekta ya uvuvi vinavyotumika katika kulinda ubora, salama na usafi wa samaki na mazao mengine ya uvuvi.
Katika sekta ya uvuvi, matumizi ya ghala la ubaridi utumika ili kulinda thamani ya samaki, kuzuia kuharibika, na kudumisha ubora wa bidhaa. Vifaa vya kuhifadhia baridi ni sehemu muhimu katika mnyororo mzima wa thamani kwa mazao ya uvuvi.
Faida za Kuhifadhi Samaki katika Ghala la Ubaridi
Kuhifadhi Ubora - Uhifadhi wa samaki katika ubaridi husaidia kulinda ubora, umbile, na ladha ya samaki, kuhakikisha kwamba wanabaki safi na kuweza kutumika kwa muda mrefu zaidi.
Kutunza thamani ya Samaki kwa muda mrefu - Hali ya joto ya chini (Ubaridi) huongeza muda wa thamani ya samaki, ambayo inamaanisha inaweza kusafirishwa kwa umbali mrefu bila kupoteza ubora wake.
Kuzuia ukuaji wa bakteria- Uhifadhi wa Samaki katika ubaridi husaidia kuzuia ukuaji wa bakteria hatari katika samaki, ambayo inaweza kusababisha uchafuzi na sumu ya chakula.
Kwa nini Utumie Maghala ya Ubaridi ya TAFICO?
TAFICO inatoa huduma bora ya kuhifadhi wa Samaki ambayo inalenga kusaidia wavuvi, wauzaji wa jumla na wauzaji reja reja kuhifadhi samaki wao katika mazingira safi na yenye ubora.TAFICO imedhamiria kukupatia huduma bora inayokidhi mahitaji yako kwa kuzingatia:
Udhibiti wa Ubora: katika suala la utunzaji, upakiaji, na udhibiti wa halijoto ambayo inahakikisha ubora na usalama wa bidhaa zako.
Uendelevu: Tunakuhakikishia huduma ya kuaminika wakati wote, tuna nafasi ya kutosha ya kuhifadhi na chanzo cha nishati cha kuaminika.