Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO)

Barafu ya Chenga

Imewekwa: 04 August, 2023
Barafu ya Chenga

Barafu ya Chenga

Barafu ya chenga ni nyembamba, inayoandaliwa kwa kuikwangua kwa namna ya vipande vidogo vya barafu vinavyonyumbulika. Sifa ya kipekee ya barafu hii ni kuongeza  thamani kwa biashara zinazotafuta suluhisho bora la upunguzaji joto na udhibiti wa halijoto. Barafu ni bidhaa yenye matumizi mengi.

 

                                                      

Matumizi ya Barafu ya chenga

Kuhifadhi mazao ya Uvuvi: Sekta Uvuvi hutumia Barafu hii ya chenga kwa ajili ya kuhifadhia mazao ya uvuvi ili kulinda  ubora na usalama wa mazao kwa ajili ya  kuhifadhi, kusafirisha, na kusindika katika uongezaji wa thamani.  

Maduka makubwa (Super Markets): Maduka ya vyakula hutumia barafu hii kwa kuhifadhi, kupanga na kuonyesha vyakula, na hivyo kuongeza mvuto wa bidhaa

                                                 

Kupooza Vinywaji: Barafu hii hutumiwa katika migahawa, baa, na maduka makubwa kwa ajili ya kupooza vinywaji inasaidia katika kuongeza  ubora wa bidhaa.

                                                         

Huduma za Afya: Hospitali, vituo vya afya na huduma ya kwanza kwenye michezo mbalimbali hutumia barafu hii  kwa madhumuni ya matibabu, kama vile kupunguza homa, maumivu ya misuli, viungo , kuhifadhi dawa na chanjo.

Ujenzi: Barafu hii ni muhimu katika ujenzi kwa ajili ya kupooza zege, ili kuhakikisha zege linakomaa vizuri na kuzuia nyufa katika miradi mikubwa.

Kemikali za Viwandani: Barafu iliyotanda hutumika katika michakato mbalimbali ya viwanda, ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa kemikali na madini, kwa udhibiti wa halijoto na matumizi ya kupoeza.

Kwa nini Utumie barafu ya TAFICO?

TAFICO imedhamiria kukupatia Barafu ya chenga 

  • Yenye ubora iliyoandaliwa kwa viwango vya juu na ufanisi mkubwa itakayo kupa matokeo ya haraka katika matumizi yako
  • Iliyozalishwa  kwa udhibiti na usafi  wa hali ya juu , na kuifanya kuwa salama kwa matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhifadhia vyakula.
  • Upatikanaji wake ni wa uhakika na kwa wakati ili kukidhi mahitaji yako.