Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO)

Majukumu ya TAFICO

 

  1. Kukuza maendeleo ya sekta ya uvuvi nchini;
  2. Kununua,kutafuta masoko,kuuza aina zote za Samaki na mazao ya uvuvi ndani na nje ya nchi;
  3. Kushiriki katika kuhamasisha uanzishwaji na uendelezwaji wa maendeleo ya uvuvi wa kitaifa na kimataifa unaolenga kuendeleza sekta ya Uvuvi na mazao yake;
  4. Kushiriki na kuhamasisha  uanzishwaji wa viwanda vya uchakataji wa samaki na kuongezwa thamani ya mazao ya Uvuvi;
  5. Kushiriki au kuanzisha ubunifu wowote wa kibiashara unaohusiana na Sekta ya Uvuvi;
  6. kuhamasisha au kufadhili tafiti zinazohusiana na sekta ya uvuvi  ikilenga kuongeza thamani ya soko la samaki, mazao ya uvuvi.