MIRADI
Katika kuvutia uwekezaji wa serikali na sekta binafsi Mpango wa Biashara (Business Plan) wa Miaka 10 umeandalia,mpango huu umeainisha miradi ya kimkakati kwa ajili ya kuongeza tija katika uvuvi wa Bahari kuu na mnyororo wa thamani wa mazao ya uvuvi . Miradi hii itekelezwa kwa kushirikiana na sekta binafsi kwa utaratibu wa Ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (Public -Private Partnership- PPP). Miradi hii itaiwezesha TAFICO kurejea katika shughuli za uzalishaji na kuimarisha sekta ya uvuvi nchini.
- Uvuvi wa Bahari Kuu kwa kutumia meli vya mishipi (Long Liner)
- Uvuvi wa Bahari Kuu kwa kutumia meli ya wavu wa kuzungusha (Purse Seine)
- Mradi wa uchakataji wa Mazao ya Uvuvi.
- Mradi wa uzalishaji barafu.
- Mradi wa ghala la ubaridi la kuhifadhia mazao ya uvuvi.
- Mradi wa utotoleshaji vifanga vya Samaki.
- Mradi wa uzalishaji wa chakula cha Samaki waafugwao.
- Mradi wa ufugaji wa Samaki kwenye vizimba. na
- Mradi wa Ufugaji wa Samaki kwenye mabwawa
UNUNUZI WA MELI YA UVUVI WA BAHARI KUU KUPITIA PROGRAMU YA ESDP/JAPAN
Shirika kupitia Programu ya Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii chini ya Serikali ya Japani (ESDP Japan) linaendelea na ujenzi wa Meli moja ya Uvuvi, ambayo ujenzi wake umefikia 75%, ikitarajiwa kukamilika na kuwasili nchini ifikapo Mwezi Disemba 2025.
Kampuni ya Ogawa Seiki ya nchini Japani inayojenga meli hiyo imekwishafanya ukaguzi wa eneo la ujenzi wa mfumo wa ufuatiliaji wa chombo (site verification) katika Makao Makuu ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) yaliyopo Ras Mkwavi, Feri- Kigamboni, ambapo utafungwa Mfumo wa Ufuatiliaji wa Chombo (Vessel Monitoring System) utakaotumika katika shughuli za meli za TAFICO.
Mfumo wa Ufuatiliaji wa Chombo (Vessel Monitoring System) ni mfumo wa mawasiliano unaotumika kufuatilia, kudhibiti na kuchunguza shughuli za uvuvi wa meli zinapokuwa baharini. Mfumo huu unatarajiwa kuanza kufungwa mwezi Septemba 2025 ili kuruhusu mawasiliano kati ya manahodha wa meli za TAFICO baharini na chumba cha udhibiti (control room) kitakachokuwa Makao Makuu.
Kukamilika kwa ununuzi na kuwasili kwa Meli hii kutaliwezesha Shirika kuanza rasmi Uvuvi wa Bahari Kuu na biashara ya samaki ndani na nje ya nchi. Kiasi cha TZS 5.9 Bilioni zitatumika kukamilisha kazi hizi.