Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO)

WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI TAFICO YA KAGAU MALI ZA SHIRIKA ZILIZOPO DAR

Imewekwa: 23 July, 2024
WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI TAFICO YA KAGAU MALI ZA SHIRIKA ZILIZOPO DAR

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) Julai 22, 2024 imefanya ziara ya kukagua mali za shirika zilizopo Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Prof. Yunus Mgaya amesema lengo la kutembelea mali hizo ni kuona hali yake na jinsi mali hizo zinavyoweza kutumika katika kulisaidia shirika kuingiza kipato.

Maeneo yaliyo tembelewa ni Kurasini, Geti namba 5 Kurasini na Ghala lililopo Chang'ombe. Maeneo mengine ni nyumba za makazi zilizopo Upanga na kiwanja na nyumba Ursino Mikocheni.

Pamoja na kutembelea maeneo hayo, Bodi pia ilikagua ukarabati wa ofisi unaondelea makao makuu ya shirika, Ras Mkwavi Kigamboni ambao ukarabati huo umefikia asilimia 95.

Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Prof Mgaya ameiagiza menejimenti kufuatilia kwa ukaribu na kuhakikisha mali hizo zinaanza kuliingizia shirika mapato, huku mali zenye mgogoro wa umiliki, zifanyiwe ufuatiliaji wa haraka kwa kuwasiliana na mamlaka husika.

“Tunaielekeza menejimenti kufuatilia kwa karibu upatikanaji wa nyaraka muhimu zitakazo wezesha upangishwaji na uendelezwaji wa mali hizi ambazo zitasaidia upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kuendesha shirika, wakati huu ambapo mchakato wa ujenzi wa meli unadendelea," amesema Prof Mgaya.

TAFICO inaendelea na mchakato wa uundwaji wa meli kwa ajili ya uvuvi wa bahari kuu, ambapo shirika linatarajia kuwa na meli tatu za kuanzia, na kwa sasa meli moja iko katika hatua ya ujenzi kupitia ufadhili wa serikali ya Japani.