Dira na Dhamira
Dira na Dhamira
DIRA
Kuwa Shirika la ushindani katika uvuvi wa kibiashara na ufugaji wa samaki Kusini mwa Jangwa la Sahara.
DHAMIRA
Kuchukua nafasi muhimu katika maendeleo ya tasnia ya uvuvi nchini Tanzania kupitia uvuvi wa bahari kuu na maji ya bara, ufugaji wa samaki na uongezaji thamani kwa maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.
MOTO
TAFICO na Uchumi wa Buluu
MISINGI YA MAADILI YETU
- Uadilifu: Wafanyakazi wa TAFICO tunatekeleza majukumu yetu kwa uadilifu wa hali ya juu, usiri na uaminifu.
- Usalama : Mazingira salama ya kazi na yenye tija ni kipaumbele chetu kwa ajili ya usalama wa wafanyakazi, wavuvi na jamii.
- Mteja kwanza: Tunatoa bidhaa na huduma kwa kuzingatia mahitaji ya mteja, bidhaa na huduma zetu zinatolewa katika ubora wa hali ya juu ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu.
- Uendelevu wa Rasilimali: Tunazingatia biashara ya kijani kwa matumizi endelevu ya rasilimali za majini na mazingira yake kwa vizazi vijavyo.
- Ukuaji: Tunahimiza maendeleo binafsi ya wafanyikazi wetu kwa maendeleo ya uendeshaji wa biashara yetu na soko kupitia ubunifu na uvumbuzi na
- Timu: Tunatumia ujuzi, maarifa na vipaji mbalimbali vya kila mtumishi ili kutimiza lengo letu kwa pamoja.