Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO)

WAZIRI ULEGA AKABIDHI BOTI KWA WAVUVI DAR NA PWANI

Imewekwa: 29 November, 2023
WAZIRI ULEGA AKABIDHI BOTI KWA WAVUVI DAR NA PWANI

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amekabidhi boti 11 kwa wavuvi wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani, katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Novemba 28, 2023.

Waziri Ulega amekabidhi boti hizo zenye thamani ya zaidi ya shilingi ya Bilioni 1. 85 zilizotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB).

"Utoaji wa boti hizi leo ni muendelezo wa uimarishaji wa sekta ya uvuvi nchini kwa kuwajengea uwezo wavuvi," Alisema Waziri Ulega.

Waziri Ulega amemuagiza Mkurugenzi wa Uvuvi nchini, Prof. Mohamed Sheikh kuhakikisha anawasilisha mkakati wa kukabiliana na uvuvi haramu nchini, mpango utakao washirikisha wadau wote muhimu wakiwemo wakuu wa wilaya.