KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA TAFICO
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imeipongeza Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kutekeleza miradi ya maendeleo inayolenga kuongeza uzalishaji na mchango katika pato la taifa.
Mwenyeketi wa Kamati hiyo Mhe. Deoudatus Mwanyika ametoa pongezi hizo Machi 10, 2026 Bungeni Dodoma kwa niaba ya wajumbe baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).
“Kama kamati tunapongeza miradi ya meli za TAFICO kwa ajili ya uvuvi wa Bahari Kuu, kamati hii imelipigania sana suala hili” alisema Mhe. Mwanyika.
Awali akitoa taarifa ya miradi inayotekelezwa na Shirika, Afisa Mtendaji Mkuu wa TAFICO CPA Shaibu Matessa amesema jumla ya ajira za moja kwa moja elfu 13,049 zitazalishwa kutokana na miradi inayoendeshwa na TAFICO, ambapo hadi sasa Shirika limenunua meli moja ya uvuvi, meli mbili zipo katika mchakato wa ununuzi kati ya meli tano zilizopangwa kununuliwa.