KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA , BIASHARA, KILIMO NA MIFUGO YARIDHISHWA NA UTEKELZAJI WA MIRADI YA TAFICO

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imesema imeridhishwa na utekelelezaji wa miradi inayoendelea kutekelezwa na Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).
Hayo yamesemwa Machi 18, 2024 wakati kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mheshimiwa Deodatus Mwanyika walipotembelea ofisi za TAFICO kujionea shughuli mbalimbali na miradi ya shirika inavyoendelea.
Akiongea katika majumuisho ya ziara ya kamati hiyo baada ya kukagua utekelelezaji wa mradi wa ukarabati wa majengo na miundombinu ya shirika, Mheshimiwa Mwanyika aliipongeza wizara pamoja na Menejimenti ya TAFICO kwa kazi nzuri inayoenedelea.
“Kamati imeona kinachoendelea, tunaipongeza wizara na watendaji wote kwa kazi hii” alisema Mwanyika.
Pamoja na utekelezaji wa miradi ya shirika, kamati hiyo imeielekeza TAFICO na wizara kuendeela kusimamia vyema utekelezaji wa miradi hiyo ambayo kukamilika kwake kuteleta tija kubwa kwa nchi, hasa ufanyaji wa shughui za uvuvi katika Bahari Kuu.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya shirika, Afisa Mtendaji Mkuu wa TAFICO, Bwana Dennis Simba aliiambia kamati hiyo kuwa shirika linatekeleza miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa majengo na miundombinu, ambao kwa sasa umefikia asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili 2024.
Pamoja na miradi hiyo, shirika linatekeleza miradi mitatu ambayo ni awamu ya pili ya Program ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (Agriculutral Sector Development Program ASDP II), Program ya Kuendeelza Uchumi na Jamii (Economic and Social Development -ESDP -Japan) na Program ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo na Uvuvi (Agriculture and Fisheries Development Program -AFDP -IFAD).
Kukamilika kwa miradi hii yote kutalisaidia shirika kuwa na meli tano za uvuvi wa Bahari Kuu, miundombinu wezeshi (maghala na magari ya ubaridi), viwanda vya kuzalisha chakula cha samaki na uchakataji wa mazao ya uvuvi.