Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO)

UJENZI MFUMO WA UENDESHAJI MELI TAFICO WAKAMILIKA

Imewekwa: 15 December, 2025
UJENZI MFUMO WA UENDESHAJI MELI TAFICO WAKAMILIKA

Ujenzi wa Mfumo wa Ufuatiliaji wa Chombo (Vessel Monitoring System [VMS]) uliokuwa ukijengwa kwenye Makao Makuu ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), umekamilika ambapo minara miwili imesimikwa na uundaji wa chumba cha mawasiliano ya redio umekamilika.

Kampuni ya Ogawa Seiki ya nchini Japani kwa kushirikiana na kampuni mbia ya ndani (Local Partner) Electricool Tanzania Limited, zimekamilisha usimikaji wa minara miwili  (Wide Band Dipole Antenna) yenye urefu wa mita 18, uundaji na ufungaji wa mfumo wa mawasiliano ya redio kwenye chumba maalum cha udhibiti (control room) ya masafa ya mbali (HF) na masafa ya karibu na ya kati (VHF), katika ofisi hizo za TAFICO zilizopo Ras Mkwavi, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Mfumo wa Ufuatiliaji wa Chombo (Vessel Monitoring System) ni mfumo wa mawasiliano unaotumika kufuatilia, kudhibiti na kuchunguza shughuli za uvuvi wa meli zinapokuwa baharini.

Mfumo huu utatumika katika mawasiliano ya Melini na chumba maalum cha udhibiti (control room).