Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO)

Je TAFICO inatoa huduma na bidhaa gani?

TAFICO kupitia utekelezaji wa miradi yake linatarajiwa kuuza huduma na bidhaa zifuatazo

  • Kuuza Samaki ndani na nje ya nchi.
  •  kuuza barafu za aina mbalimbali
  • Kutoa huduma ya kuhifadhi Samaki kwenye maghala ya ubaridi.
  • Kutoa huduma ya uchakataji wa mazao ya uvuvi kwenye viwanda vyake.
  • Kutoa huduma ya usafirishaji wa mazao ya uvuvi kwa kutumia gari la ubaridi.
  • Kutoa huduma ya kuzalisha na kusambaza vifaranga vya Samaki.
  • Kutengeneza na kuuza chakula cha Samaki.