TAFICO ni Nini?
TAFICO ni Nini?
Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) taasisi ya Umma iliyoanzishwa mwaka 1974 chini ya Sheria ya Mashirika ya Umma Na. 17 ya mwaka 1969. TAFICO inajukumu la kuendeleza sekta ya uvuvi nchini kupitia uwekezaji katika miradi mbalimbali inayolenga kuongeza tija hasa katika uvuvi wa Bahari kuu na kuimarisha mnyororo wa thamani kwa mazao ya uvuvi. TAFICO inatafanya shughuli zake katika ukanda wa Bahari ya Hindi, Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika, Ziwa Nyasa na maji madogo.