Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO)

AGRF

05 September, 2023 - 08 September, 2023
08:00:00 - 04:00:00
JNICC Dar Es Salaam
barua@tafico.co.tz

                                                MKUTANO WA AGRF 2023

Africa Green Revolution Forum (AGRF) ni Jukwaa la Mapinduzi ya Kijani Afrika, liliundwa kwa lengo la kuweka mikakati ya kuimarisha sekta ya kilimo mazao. Hata hivyo, katika mkutano wa AGRF uliofanyika mwaka 2022, Kigali Rwanda, iliazimiwa kuhuisha jina hilo kutoka Jukwaa la Mapinduzi ya Kijani Afrika na kuwa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (Africa Food System Forum). Mabadiliko haya yalilenga kuongeza wigo wa ushiriki wa sekta mtambuka za mifumo ya chakula zikiwemo sekta za mifugo na uvuvi.

Kwa mwaka 2023 Tanzania imebahatika kuwa nchi ya kwanza kuwa mwenyeji wa mkutano huo baada ya mabadiliko haya. Mkutano huo mkubwa wa kimataifa unatarajiwa kufanyika hapa nchini tarehe 5-8 Septemba, 2023 jijini Dar es salaam na utaongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkutano huu utatoa fursa adhimu kwa  wadau wa sekta za Mifugo na Uvuvi   kukutana na wafanyabiashara mashuhuri na wawekezaji kutoka katika nchi mbalimbali ulimwenguni, hivyo itasaidia kufungua milango ya uwekezaji, masoko, kukuza mitaji na kuongeza ushirikiano wa kibiashara kwa wadau. Mkutano huo pia utatoa fursa za kuona ubunifu na teknolojia mbalimbali ambazo zinaweza kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao ya mifugo na uvuvi.

Vilevile, jukwaa hilo linatoa fursa kwa wafanyabiashara kufanya maonesho katika eneo la mkutano kwa lengo la kuonesha shughuli zinazofanyika katika minyororo ya mifumo ya chakula nchini.

AGRF